Hata hivyo amedai kuwa ana kazi kubwa kuweza kuupiku wimbo wake uliopita.
Hemedy ambaye kwa sasa anatamba na video ya wimbo, Imebaki Story, ameiambia E-Newz ya EATV kuwa anajipanga kufanya kitu kikubwa zaidi.
“Nashukuru Mungu kazi yangu ‘Imebaki Story ‘ imepokelewa vizuri, kwa sababu ndani ya muda mfupi tu watu wengi wamekuwa wakiizungumzia, so sasa hivi nina kazi kubwa na kuipiku hii ngoma,” alisema. “Kwahiyo najiandaa sasa hivi nipo jikoni na track yangu mpya inakuja inaitwa Some Day ambayo nimemshirikisha Mr Blue. Na tunapozungumza zimebakia siku 40 hiyo track itakuwa inatoka, kwahiyo ni kitu kingine kikubwa kinakuja, video yake ni kubwa. Halafu najaribu kuandika script ambayo itajaribu kuipiku video iliyopita na italeta taswira nzuri kwenye macho ya watazamani. Kwahiyo Some Day, coming soon! Mashabiki wangu wategemee kitu kikubwa kutoka kwangu.”
0 comments:
Post a Comment