Mwana FA aeleza kwanini anahofia kutoa wimbo mpya kwa sasa

Binamu

Mwana FA a.k.a Binamu ni miongoni mwa wasanii ambao wanahofia kutoa kazi mpya kwa sasa.

“Ebana saizi kila mtu siasa, kwahiyo nina ngoma ndani lakini naona kama ntapoteza muda ntatumia nguvu nyingi sana kufanya watu wasikie” amesema Binamu kupitia 255 ya XXL.
“…kwasababu naona concentration yote imeenda kwenye siasa, hata ya kwangu mwenyewe iko kwenye siasa. Kwahiyo nawapa watu muda ngoja mambo yatulie kidogo yakitulia katikati wakati wa kampeni itakuwa poa kama hayatatulia tusubiri uchaguzi ukiisha tutatoa ngoma, zipo tu hazichachi.”

Wasanii ambao wameendelea kuachia kazi mpya katika kipindi hiki ni pamoja na Jux ambaye ameachia video mpya ‘Looking For You’ hivi karibuni, Bonta aliyeachia ‘Mapenzi Matamu’, Damian Soul ft. G-Nako ameachia ‘Tudumishe’ pamoja na Nuru the Light anayetarajia kuachia wimbo/video mpya ‘L’ siku chache zijazo.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment