‘Nana’ ya Diamond yakamata namba 1 kwenye DNA Top 5 ya BBC Radio 1Xtra ya UK


Inatia moyo kuona nyimbo za wasanii wa Tanzania zinafanya vizuri kwenye chati mbalimbali za vituo vya Radio na Tv ndani na nje ya Afrika.
Diamond

Tumeshuhudia kazi za wasanii wa Bongo akiwemo Diamond, Vanessa Mdee, Alikiba, Joh Makini, Navy Kenzo ziking’ara katika chati za vituo tofauti.
Wimbo wa Diamond aliomshirikisha staa wa Nigeria Mr Flavour, ‘Nana’ umekamata namba 1 kwenye DNA Top 5 ya BBC Radio 1Xtra ya Uingereza inayoendeshwa na Dj Edu.
Kituo hicho kimempongeza Diamond kupitia Twitter kwa kushika namba 1:

Hii ni chati nzima ya DNA Top 5 ya wiki hii, 24 August 2015
1. Diamond ft. Flavour – Nana
2. Patoranking ft. Wande Coal – My Woman, My everything
3. Wizkid ft. Drake & Skepta – Ojuelegba Remix
4. Khulichana ft. Patoranking – No Lie
5. Davido ft. Meek Mill – Fans Mi


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment