Muziki wa Bongo unaendelea kukua siku hadi siku na kutambulika kimataifa, kutokana na kazi za wasanii wetu kuendelea kushika chati mbalimbali kwenye vituo vikubwa vya kimataifa hadi kufika nafasi za juu.
MTV Base wana chati ya video 10 za Afrika iitwayo Official African Chart, na miongoni mwa video zilipo katika chati hiyo wiki hii, 4 ni za wasanii wa Tanzania.
Producer Nahreel ana kila sababu ya kufurahia mafanikio hayo kama Mtanzania, lakini anayo sababu nyingine ya kutabasabu kwasababu wimbo wao ‘Game’ ni miongini mwa video bora 10 Afrika kwa sasa, na anayo sababu ya ziada ya kujivunia kwasababu yeye ndiye producer aliyetengeneza nyimbo zote nne za wasanii wa Tanzania zilizoko kwenye chati hiyo.
Hizi ni nyimbo 4 zilizoko kwenye African Chart Top10 ya MTV Base wiki hii:
Nafasi ya 1 imekamatwa na Diamond ft. Flavour wimbo ni ‘Nana’
Nafasi ya 5 imekamatwa na Navy Kenzo ft. Vanessa Mdee wimbo ni ‘Game’
Nafasi ya 7 ni Joh Makini ft. G-Nako wimbo ni ‘Nusu Nusu’
Na Bonus track ni video mpya ya Jux ft. Joh Makini wimbo ni ‘Looking For You’.
Nahreel amezungumza na Bongo5 na kuelezea furaha aliyonayo kwa mafanikio hayo;
“Kwakweli najisikia vizuri sana, kwanza inaniongezea nguvu ya kuendelea kufanya kazi zaidi, kwasababu nguvu nayoiweka ni kubwa na unajua unapoweka nguvu halafu unaona matunda yake inakupa nguvu sana… tutaendelea kuweka juhudi mpaka hapo tutakapohakikisha MTV nzima kuna nyimbo 10 za Tanzania.” – Alimaliza Nahreel.
0 comments:
Post a Comment