Rappers wa Kike wa Bongo wakiongozwa na Witnes waanzisha umoja wao ‘Female Rappers Empowerment’-FRE



Ma-rapper wa kike wa Bongo wameanzisha umoja wao utakaowaunganisha katika maswala mbalimbali yanayohusiana na muziki wa Hip Hop kwa wasanii wa kike.
Witnesz

“Tumeanzisha umoja wa ma-rapper wa kike ambao tunajiita ‘FRE’ ama unaweza kusema Female Rappers Empowerment,” alisema Witnes kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm.
Witnes amesema kuwa wakati umoja huo unaanzishwa Jumamosi iliyopita walikuwa rappers wa kike 11 lakini hadi sasa wameendelea kuongezeka na kufika 17.
“Lengo kuu la hili kundi ni kwaajili ya kuangalia namna gani rappers wa kike tunaweza tukafanya vizuri kwenye industry.”

Witnes amewataja members wa kundi hilo kuwa ni Chiku Keto, Chemical, Cindy Rulz, Ice Baby, Illu da crazy Flow, P Tiffah, Natty E, Petrina, Phine, Pinky, Sista P, Stosh, Tammy the baddest, Tiffah, Shanti verurio pamoja na Witnes mwenyewe.
Kibonge mwepesi ameongeza kuwa miongoni mwa malengo ya kuanzisha umoja huo ni pamoja na kubadilishana uzoefu.

“…vile vile kwasababu kuna mchanganyiko wa rappers wa zamani na rappers wa sasa, so rappers wa zamani watakuwa wanashea uzoefu ambao walishawahi kufanya vizuri na ambao walijaribu kutaka kufanya na ambao wapo sasa hivi tunashea uzoefu kwenye kundi.”


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment