Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EATV, Roma amesema kinachotakiwa ni kuhakikisha show yake inaenda vizuri.
“Kuna watu wanaamini akipata pombe ndio anapata mzuka na hiyo ipo toka enzi hizo,” amesema rapper huyo. “Kwahiyo hata bongo kuna wasanii wanafanya hivyo ili kupata vibe na anafanya poa. Sema ni ile mentality ya mtu ambayo amejiwekea, ukienda hata kwa wafanyakazi hasa hasa wajenzi wenyewe mpaka waonje kwanza ndo wanafanya kazi kwa nguvu. Hata madaktari baadhi yao hawaingii kwenye operation mpaka apate kitu ambacho kitampa vibe ya kufanya kazi yake kwa umakini,” ameongeza.
Unakubaliana na mtazamo wa Roma?
0 comments:
Post a Comment