Picha: Weusi wamfuata AKA Afrika Kusini kushoot video ya ngoma waliyomshirikisha





May mwaka huu rapper wa Afrika Kusini, AKA alitua jijini Dar es Salaam kwa mwaliko wa Diamond Platnumz kwenye Zari All White Party ambapo alitumbuiza pia.


Joh Makini na G-Nako wakiwa na mwenyeji wao, AKA
Weusi walitumia nafasi hiyo kurekodi ngoma waliyomshirikisha rapper huyo. Nahreel ndiye aliyesimamia utayarishaji wake.


G-Nako na AKA
Na sasa Joh Makini na G-Nako wamesafiri hadi jijini Johannesburg, Afrika Kusini kwenda kushoot video hiyo.


Weusi wakiwa location?

Wawili hao wamekuwa wakishare picha zinazowaonesha wakiwa kwenye maeneo mbalimbali jijini humo wakiwa na AKA. Wameshare pia kipande cha video kinachomuonesha AKA akiwazungusha kwenye mitaa ya jiji hilo.



Picha zinaonesha kuwa tayari wameshoot video hiyo na licha ya kutomtaja muongozaji, hakuna shaka kuwa ni Justin Campos, aliyeshoot video ya Nusu Nusu.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment