Ile ahadi aliyoitoa mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe, Said Fella kupitia Bongo5 kuwa Yamoto Band wamepata mwaliko wa kwenda kuwaburudisha Watanzania na wana Afrika Mashariki waishio Marakeni imetimia.
Promota maarufu DMK ambaye amekuwa akipeleka wasanii wengi kufanya maonesho Marekani, ikiwa ni pamoja na ile show ya Ommy Dimpoz na Shilole inayotarajiwa kufanyika Septemba 5, 2015, ameshare poster ya show ya Yamoto Band itakayofanyika katika jiji la Kansas Novemba 27, 2015.
Fella amesema kuwa wakiwa huko Yamoto wanatarajiwa kufanya show katika miji mitatu. Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Yamoto Band kufanya ziara nchini Marekani.
0 comments:
Post a Comment