'Viagra' ya wanawake yazinduliwa Marekani

Shirika la Dawa na Chakula nchini Marekani (FDA) limeidhinisha matumizi ya dawa ya kwanza kabisa iliyoundwa mahususi kuwatibu wanawake ambao hawana hamu ya kufanya mapenzi maarufu ''viagra ya wanawake''



Dawa hiyo inaviungo maalum vinavyofanya kazi kwa kuongeza kemikali fulani akilini mwa wanawake ilikuimarisha hamu ya kutaka kufanya mapenzi

Flibanserin inayotengezwa na kampuni ya kutengeneza madawa ya Sprout Pharmaceuticals imeidhinishwa na FDA

Sampuli moja ya dawa hiyo itakuwa ikiuzwa kwa jina "Addyi" katika maduka ya madawa japo iliwasilishwa kwa shirika hilo la FDA na kukataliwa.

Dawa hiyo ilikataliwa mara mbili kwa sababu ilikuwa inasababisha watu walioimeza kusinzia mbali na visa kadha vya kuzirai

Wanawake waliojaribu dawa hiyo wameripoti ''kufikia kilele'' takriban mara moja kwa mwezi.
Awali dawa hiyo ilikuwa ikitengenezwa na kampuni ya kuunda madawa ya Ujerumani, Boehringer Ingelheim

Lakini Sprout iliinunua baada ya kushindwa kuidhinishwa nchini Marekani mara mbili.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa shirika hilo la FDA, dawa hiyo imeundwa mahsusi kutibu ukosefu wa hamu ya kufanya mapenzi kwa wanawake

'hypoactive sexual desire disorder (HSDD)'.

Dawa hiyo hata hivyo itapeanwa baada ya kupata ushauri wa daktari.
Madaktari wanatarajiwa kutoa dawa hiyo kwa wagonjwa wa ''female sexual interest ama arousal disorder (FSIAD)

Lakini dawa hiyo itaambatana na onyo kali la kiafya kuhusu uwezekano wa mwanamke kupata madhara ikiwa ataimeza pamoja na pombe

Mojawapo wa mashirika ya kutetea haki za wateja limeunga mkono hatua hiyo lakini Shirika lingine limesema dawa hiyo ni hatari kwa wanawake
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment