Mambo 10 unayo takiwa kuacha kufanya maishani mwako




Ili kufanikiwa kwenye maisha kuna mambo mengi ambayo yanaaminika ukiyafanya ni lazima tu utafanikiwa. Wapo wanao amini kuwa kuna uchawi ndio maana mtu hafanikiwi, Wapo wanao amini ni laana ndio maana mtu hafanikiwi, nk. Ila kuna mambo ambayo tumekuwa tukiyafanya wenyewe mara kwa mara na kupelekea kushidwa kufikia malengo yetu.

Haya ni mambo kumi 'TOP 10' ambayo unatakiwa kuacha kufanya.

1: Acha kupoteza muda wako na watu wasio sahihi.

Maisha ni mafupi sana kwa kupoteza muda na mtu ambaye ananyonya furaha yako. Kama mtu anakuhitaji kwenye maisha yao basi atatengeneza nafasi ya wewe kuwepo kwenye maisha yake, Hutakiwi kupambana ili kuwa na mtu. Kamwe usithubutu kupoteza muda wako kwa mtu ambaye anadharau thamani yako.

Kumbuka, Sio mtu anaye simama na wewe wakati wa raha kuwa ndiyo rafiki kwako, bali yule anaye simama na wewe wakati wa shida yako huyo ndiye rafiki wa kweli.


2: Acha kukimbia matatizo yako.Mbambana nayo uso kwa uso, Japokuwa huwa magumu.

 Sio kila ambaye yupo kwenye mafanikio amefanikiwa kwa asilimia zote kuyashinda matatizo ambayo alikutana nayo, La! Ila yamekuwa ni chachu ya yeye kugundua njia nyingine zaidi za kufanikiwa ki maisha. Kumbuka tumeubwa kuwa wa kukwazika, kukasirika, kusukwa sukwa na kushindwa. Kwasababu hiyo ndiyo njia pekee ya kupambana na matatizo, kujifunza, kuyaelewa na kuyasuluhisha na kuyashinda.


3: Acha kudanganya nafsi yako.

Unaweza kumdanganya mtu yoyote kwenye ulimwengu huu, Lakini huwezi kuidanganya nafsi yako. Maisha yetu yanaendelea pale tu tunapo amua kuchukua fursa, Na chakwanza na kigumu kuliko vyote ni kuwa wawazi kwenye nafsi zetu.


4: Acha kujifanya kuwa mtu ambaye siyo wewe 'Jikubali'.

Moya ya changamoto kubwa kwenye maisha ni kuwa wewe 'Being yourself' au kujikubali. Usijibadilishe hivyo watu watakupenda. Kuwa wewe 'jikubali' na watu sahihi watakupenda wewe 'The real you'.


5: Acha kufikiri kuwa haupo tayari.

Hakuna ambaye anajisikia 100% wakati nafasi inapo jitokeza. Kwakuwa nafasi za pekee zinazo tokea duniani hutokea kwa kushtukiza na wakati tunajiona hatuwezi, ambapo hutufanya kuto jisikia sahihi.


6: Acha kukataa mahusiano mapya kwakuwa yaliyo pita yalikuacha na maumivu.

Katika maisha utatambua kuwa kuna makusudio kwa kila binadamu ambaye unakutana naye. Yupo atakaye kwambia, Yupo atakaye kutumia na yupo atakaye kufundisha. Lakini lamuhimu, yupo atakayekuwa wa pekee kwako.


7: Acha mashindano na kila mtu.

Usihofu kwa vitu ambavyo wengine wamekuwa wanafanya bora zaidi yako. Tazamia kwenye kushinda yale uliyo panga kuyashinda kila siku. Mafanikio ni juu yako na nafsi yako pekee.


8: Acha kupoteza muda kujielezea mambo yako kwa wengine.

Walio marafiki zako hawalihitaji hilo na walio maadui zako pia hawaliamini hilo. Unachotakiwa kufanya ni kile unachodhani ni sahihi kwenye maisha yako.


9: Usijifanye kuwa kilakitu kipo sawa wakati mambo si sawa.

Ni sawa ku shindwa kwa kipindi fulani. Hutakiwi kila wakati kujinadi/kujifanya kuwa wewe ni makini, na wala haihitajiki kupoteza wakati kuthibitisha kuwa kila kitu kipo sawa. Hutakiwi kushughulika na nini watu wengine wanafikiri pia, Lia kama inakubidi kulia, ni afya kutokwa machozi.

Kabla sijafika kwenye namba 10, Hizi ni bonus.
Usilaumu wengine kwa matatizo yako.
Acha kutaka kuwa kila kitu kwa kila mtu.
Acha matamanio ya kitu kidogo na kuacha jambo kubwa.
Acha kufanya jambo moja hilo hilo miaka nenda rudi.
Acha kutazamia kwa jambo ambalo hutaki litokee.
10: Ondo wasiwasi/Usiogope.

Hofu haitaondoa mateso ya kesho, Itaondoa furaha ya kesho. Njia sahihi ya kupambana na hofu ni kujiuliza mwenyewe: "Jambo hili litadumu kwa mwaka mzima? Miaka mitatu? Miaka mitano? Kama siyo basi huna sababu ya kuwa na hofu juu ya jambo hilo.

Hizo ni Top 10 zangu za leo, Wewe ipi umeipenda? Nitupie comment yako hapo chini juu ya Top 10 za leo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment