Nimekuja na ‘modern mduara’ – AT

Muimbaji mwenye asili ya visiwani Zanzibar na mkali wa muziki wa mduara, AT, amesema kazi yake mpya iitwayo Mama Mie ni kazi inayodhihirisha mabadiliko aliyoyaleta kwenye muziki wa mduara.

AT


AT amesema mtindo anaofanya sasa ni modern mduara.
“Nimefanya mduara ambao upo kimodern zaidi ambao unaweza kumvutia mtu yeyote na kuona kumbe anaweza kufanya kazi na mimi kwa kuwa njia hii niliyoitumia ni rahisi zaidi ambayo mtu yeyote anaweza kuingia na tukafanya kazi,” AT aliiambia EATV.

“Na kingine ambacho nimefanya, ni kuonesha kuwa nchi yetu bado ni nzuri na ina maeneo mengi ya kufanyia video. Inabidi wasanii wa Tanzania kutulia na kufanya video hapa hapa ili kutangaza nchi yetu. Bado ina maeneo mengi sana. Kama hii video ambayo nimefanya mimi imeonesha kuwa bado tuna maeneo ya kutosha na kutangaza utalii wa nchi yetu,” alisisitiza.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment