Nimesikitishwa na uzushi kuwa huwa naandikiwa mashairi yangu – Stamina




Hakuna kitu kinachomkera rapper kama kuambiwa kuwa huandikiwa mashairi na mtu mwingine (ghost writer). Hiyo ilikuwa ni chanzo cha beef iliyokwisha ya Drake na Meek Mill. Meek alidai kuwa Drake anaandikiwa mashairi na mtu. Tetesi kama hizo zimemkumba pia Stamina.



Akizungumza Bongo5, Stamina amesema amesikitishwa na uzushi huo na kwamba watu walioamua kutangaza taarifa hizo, walikuwa wanahijati ‘kiki’ kipitia jina lake.

“Kuna taarifa ilitoka ambayo sikuipenda,” amesema. “Kuna mtu alirekodiwa akasema Stamina anaandikiwa mistari. Hakuna taarifa iliyoniudhi duniani kama ile na nilimpigia simu yule dogo aliyerekodiwa akasema yeye alisikia story mtaani eti msanii anayeniandikia mistari ni Mash J,” ameongeza.

“Nikampigia huyo Mash J na yeye anashangaa hizo taarifa na amesema hajaongea sehemu yoyote. Kwahiyo nikagundua kuna watu wanatafuta kiki kwa lazima halafu bahati mbaya kiki ikagoma.”

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment