Usher afunga ndoa kimya kimya na meneja wake Grace Miguel


Usher Raymond amerudisha tena title yake ya kuwa mume wa mtu, baada ya kufunga ndoa na girlfriend wake wa muda mrefu Grace Miguel, ambaye pia ni meneja wake.



Tetesi za Usher kufunga ndoa zilianza baada ya kuonekana akiwa amevaa pete ya ndoa ya dhahabu alipokuwa vacation huko Havana, Cuba, na baadae E! Online walithibitisha uvumi huo kwenye county ya Fulton huko Georgia ambako cheti cha ndoa yao kilitolewa mwezi huu.



Usher mwenye umri wa miaka 36 na Grace mwenye umri wa miaka 45, wamekuwa kwenye uhusiano kuanzia mwaka 2009, na waliingia kwenye uchumba January mwaka huu.

Usher na aliyekuwa mke wake Tameka Foster waliachana mwaka 2009, baada ya kufanikiwa kupata watoto wawili kwenye ndoa yao iliyodumu kwa miaka miwili.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment