Zuma afanya mashauriano na Bashir-Beijing


Rais Omar al Bashir na viongozi wengine wa Afrika
Huku uchina ikiadhimisha miaka sabini tangu ilipoishinda Japan katika vita vya pili vya dunia, marais wa Afrika Kusini na Sudan, ambao wanahudhuria sherehe hizo, wamefanya mkutano wa ghafla kujadili uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Mara ya mwisho wawili hao wakikutana, kiongozi wa Sudan Omar al Bashir, alikuwa akihudhuria mkutano wa wakuu wa serikali wa Muungano wa Afrika AU, mjini Johannesburg Juni mwaka huu.

Lakini kiongozi huyo aliondokwa kwa ghafla baada ya shirika moja lisilo la kiserikali kwenda mahakamani, kutaka kiongozi huyo wa Sudan akamatwe na kuwasilishwa kwa mahakama ya kimataifa ya ICC.

Bashir anakabiliwa na mashtala ya mauaji ya halaiki na uhalifu wa kivita ambao ulisababisha vifo vya zaidi ya watu laki tatu.

Mkutano huo sasa umeashiria kuwa kesi hiyo iliyowasilishwa mahakamani nchini Afrika Kusini, ya kutaka kiongozi huyo wa Sudan akamatwa haijaadhiri uhusiano kati rais Omar al Bashir na rais Jacob Zuma.

Taarifa kutoka kwa ofisi ya rais Zuma imesema kuwa wawili hao walijadili masuala kadhaa ikiwemo kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

Sudan na Afrika Kusini zimesaini mikataba 16 ya ushirikiano katika secta ya kilimo, nishati, miundo mbinu, sayansi na technolojia.

Rais Zuma pia amekubali mwaliko wa rais Bashir kuzuru Sudan.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment