Vanessa Mdee ataja sababu za kuchelewa kuitoa album yake ‘Money Mondays’



Album ya Vanessa Mdee, ‘Money Mondays’ ni kama imekamilika tayari lakini muimbaji huyo amesema ameichelewesha kuitoa kwasababu anaitengenezea mkakati mzuri wa kuichia.



Vanessa ameiambia Bongo5 kuwa anaangalia njia sahihi ya kuitoa.

“Naichelewesha kuitoa sababu natafuta proper distribution plan,” amesema.

“Sitaki tu itoke halafu watu wakasikiliza halafu ikabakia hamna faida yoyote tuliyotengeneza. Nataka kutumia fursa kutengeneza album ambayo italeta utofauti kwenye utoaji wa album. Kwasababu kwenye masuala ya muziki tuko vizuri lakini tunasambazaje? Je tukisambaza tunategemea kupata faida gani?, tuna make sure vipi inafika kote kule inakotakiwa kufika?, Kwahiyo hivyo ni vitu ambavyo navifanyia kazi kabla sijaitoa,” ameongeza.

“Otherwise inaendelea vizuri na album itakuwepo very soon.”

Vanessa kwa sasa anafanya vizuri Afrika nzima na wimbo wake ‘Never Ever.’

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment