Nikki Wa Pili: Najipanga kufanya video kubwa ya ‘Baba Swalehe’ na director mkubwa wa nje
Baada ya Joh Makini kufanya video mbili (Nusu Nusu na Don’t Bother), na G-Nako kufanya video moja (Original) Afrika Kusini na muongozaji Justin Campos, sasa ni zamu ya Nikki kufanya video na muongozaji huyo ambaye ameonekana kukubalika sana na wasanii wengi wa Bongo wanaomkimbilia kufanya naye kazi kwa sasa.
Rapa wa Weusi Nikki Wa Pili ameieleza Bongo5 kuwa anajiandaa kufanya video kubwa ya wimbo wake mpya ‘Baba Swalehe’, na mpango wake ni kufanya na director wa nje.
“Baba Swalehe’ najipanga nataka nifanye video kubwa, kwasababu imeshakuwa nyimbo kubwa, nafikiria kufanya na director mkubwa naweza nikafanyia nje au..kwa sababu pia nilipata tetesi kwamba Campos alikuwa na mpango wa kuja huku mwezi wa 12 Tanzania, kwahiyo kama atakuja naweza nikafanyia hapa pia.” Alisema Nikki.
Kuhusu kwanini alichelewa kuamua kufanya video nje kama wenzake Joh na G-Nako:
“Lakini kiukweli nimekuwa nikijifunza, ujue ni vizuri ufanye video iwe kama ya kwenda step lakini usifanye video kama njia ya kukimbia kutengeneza audio nzuri. Na nimeshaona baadhi ya wasanii ambao wamefanya video kwangu mi nimeona hazijawasaidia wamefanya video kubwa South Afrika lakini kwasababu hawakuwa na audio nzuri, mimi ntafanya video kubwa lakini mimi naamini kwanza msingi wa kwanza ni kutengeneza audio nzuri , audio ikishakubalika sana ndio unafanya video, au hata kama unafanya vyote kwa pamoja lazima uhakikishe kwamba audio kali.” alifafanua Nikki.
Ameongeza kuwa kilichomkwamisha kufanya video ya wimbo wake ulipita ‘Safari’ ni mazingira ya watu aliowashirikisha.
“Kwa mfano Jux alikuwa yuko China, Vee Money alikuwa anasafiri sana, kwahiyo mazingira kama hayo pia yalikwamisha utengenezaji wa video ya Safari”. Alimaliza Nikki.
0 comments:
Post a Comment