Kazi iliyompeleka mshindi wa Airtel Trace Music Star, Mayunga Nalimi nchini Marekani, ya kufanya collabo na boss wa label ya Konvict Music, Akon imekamilika.
Mayunga ameelezea jinsi kazi hiyo ilivyofanyika kwa siku moja, kuanzia kupewa wimbo kuushika, kurekodi na kushoot video vyote ndani ya saa 24.
“Nilikua nina siku moja tu yakushika kila kitu kwenye wimbo niliopewa” Mayunga ameiambia TeamTz “Kwahiyo ilinibidi nijitume ili niufahamu vizuri wimbo ili nifanye kitu kizuri hata bwana Akon afurahi na namshukuru Mungu alifurahi sana”
Mayunga ambaye kabla ya kurekodi alipata muda wa kupewa ushauri na mafunzo na Akon, ameongeza kuwa baada ya kumaliza kurekodi audio walishoot video siku hiyo hiyo huko Hollywood, na mrembo aliyepewa kama video model aliwahi kuwa main character kwenye video ya Chris Brown.
“Huyo video queen ni mkubwa sana kwani amewahi kufanya video ya Chris Brown kama Main character” Amesema Mayunga
Hizi ni baadhi ya picha za BTS
Source: Team Tz
0 comments:
Post a Comment