Fabregas hajui nini tatizo katika klabu yake Chelsea kuhusu matokeo mabaya
Kiungo Cesc Fabregas wa Chelsea na timu ya taifa ya Hispania ameelezea hasira kutokana na matokeo duni ya klabu ya Chelsea msimu huu kwao umekua mbaya sana na kwamba hajui nini kinaenda vibaya katika kikosi hicho cha kocha Jose Mourinho.
Akiongea kwa uchungu sana na Gazeti la kihispania Marca., Cesc ameonesha kukasirishwa sana na jinsi msimu unavyoenda huku akisema matokeo hayawatendei haki kwani wanacheza vizuri kuliko matokeo wanayopata uwanjani.
”Kwa hakika sifahamu ninikimetusibu msimu huu”
Mabingwa hao watetezi wamepoteza mechi 7 kati ya 12 walizocheza msimu hu.
The Blues’ wana alama tatu tu zaidi ya timu zinazotishiwa kushushwa daraja.
‘Sijui nini kinaendelea ,,,tumekuwa tukicheza vyema ila hatuna bahati ya kufunga bao’ alisema kiungo huyo.
‘Kwa wakati mwengine,huwa ukidana mpira na uguse kidogo unapaa na kuingia ,lakini hivi sasa hata ukifumua mkwaju unakwenda nje’ Fabregas alisema.
‘Tunahitaji kuanza kushinda mechi zetu kwa udi na uvumba la sivyo haitukuwa vyema’
Kiungo huyo wa timu ya Uhispania ni mmoja kati ya wale wanaolaumiwa na kocha Jose Mourinho kuzembea msimu huu.
Majuma mawili yaliyopita Fabregas alikanusha kuwa wachezaji wanafanya mgomo baridi dhidi ya kocha wa Chelsea Mourinho.
Fabregas alisema kuwa anafurahia sana uhusiano wake na meneja huyo.
0 comments:
Post a Comment