Mwana FA adai Hip hop imepoteza maana yake
Mwana FA amesema hawezi kuwaunga mkono wasanii wanaopoteza misingi ya muziki wa Hip Hop kwa sababu ya kutengeneza pesa na kuacha changamoto zinazowakabili watanzania
Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, FA alisema sio lazima kwa msanii kufanya kitu ambacho hana uhakika nacho, hata kama kinaingiza pesa nyingi.
“Iko so obvious muziki umebadilika sana, umetoka katika ile misingi iliyowekwa na sababu zake za kuwepo, umekuwa kuhusu starehe na hela peke yake. Yaani ile misingi imebadilika sana, na vitu vingi ambavyo vilikuwa vinapingwa vilionekana vya kipumbavu mwanzoni huko, sasa hivi ndio kama style, yaani vile vitu ambavyo vilikuwa vinapingwa ndio ambavyo watu wanafanya kwa sababu watu wanataka kutrend watengeneze hela”, alisema Mwana FA.
Aliongeza, “Muziki umekuwa biashara kiukweli, kama unaleta hela why not watu wachukue hela zao, lakini ninachopinga ni kuipoteza kabisa Hip Hop kwa sababu ya hela. Kuna vitu vingi vya kufanya na bado ukapata mkate wako wa kila siku, sio lazima usingizie unafanya hii aina ya muziki tunayoifanya wakati huna talent hiyo, sio lazima kujisingizia kufanya kitu ambacho huna uwezo nacho ili tu uingize hela”, aliongeza Mwana FA.
0 comments:
Post a Comment