Kala Jeremiah: Ukifanya video nje huku unategemea show za ndani ni kula hasara


Kuna baadhi ya wasanii wa Bongo ambao waliwahi kusema hawana mpango wa kwenda kushoot video zao nje ya Tanzania, lakini baadae walibadili mawazo na kwenda kushoot huko.



Miongoni mwa wasanii waliobadili mawazo ni Ben Pol, ambaye hivi karibuni ameshoot video mpya Afrika Kusini na Justin Campos.

Kala Jeremiah pia aliwahi kusema hafikirii kwenda kushoot video nje, na sababu aliyoitoa ni kutokana na nyimbo zake nyingi zinazungumzia matatizo ya jamii za Kitanzania.

Bongo5 ilimtafuta Kala kutaka kufahamu kama bado anasimamia msimamo huo licha ya ongezeko kubwa la wasanii kwenda kushoot video nje.

“Kushoot video nje lazima kuwe na sababu za msingi.” Kala alianza kwa kujibu hivyo.

“Sababu kuu inaweza kuwa ni kwakua umefanya wimbo husika na msanii wa nchi hiyo waweza kwenda maana ni ngumu yeye kukufuata. Lakini kwa kujidanganya kwamba ili mziki wako ukubalike kimataifa ni lazima ufanye video nje ni kupoteza muda na pesa, maana location zote nzuri na zinazoweza kuwashtua watu wakaona wameona kitu kipya ziko kwetu. “ alieleza Kala.

Pia ameongeza kuwa kuna wasanii ambao wameshoot video nje lakini bado hawajafanikiwa kupanua soko la kazi zao, kwani bado wanafanya show zile zile za ndani na kuondoa maana ya kufanya video nje ili kupanua soko hasa kupata shows za kimataifa.

“Na pia wapo wasanii wengi walifanya video nje kwa gharama kubwa lakini wanarudi nakusubiria show zilezile za mwanza na arusha ambazo tunaenda nao na inawezekana mimi nimelipwa zaidi yao. Mi nadhani ukifanya video nje lazima uwe na uhakika wa kufanya show nje pia lakini kama unategemea show hizi hizi za ndani unakula hasara maana kanuni ya biashara ni faida inayofanana na mtaji.´alimaliza Kala ambaye anajiandaa kuachia wimbo mpya mwezi ujao.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment