Wema Sepetu kuisaliti ndoa yake kwenye ‘Chungu Cha Tatu’
Wema Sepetu amevaa uhusika kwenye filamu ya Chungu Cha Tatu kama mwanamke aliye ndani ya ndoa lakini anashindwa kujizuia na kuamua kutoka na wanaume wengine ili kukidhi mahitaji yake.
Akizungumza na Bongo5, afisa masoko wa kampuni ya Steps Entertainment, Kambarake alisema filamu hiyo italeta msisimko kutokana na mwanadada huyo kuivaa vyema uhusika wake.
“Wema ndio mhusika mkuu na ameingia kwenye mahusiano anajikuta anaingia kwa mwanaume fulani labda atapata anachohitaji. Kwahiyo mapenzi katika watu wa tatu ndio Chungu cha Tatu. Ndani yupo JB, Pacho Mwamba na wengine,” alisema.
Filamu hiyo itatoka December mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment