Jay Z na Beyonce washinda kesi ya kuhusiana na wimbo wao ‘Drunk In Love’



Jay Z na Beyonce wameshinda kesi iliyofunguliwa na muimbaji wa Hungary aliyedai kuwa wanandoa hao walitumia sauti yake kwenye wimbo wao ‘Drunk In Love.’



Muimbaji huyo aitwaye Mitsou aliwashtaki The Carters kwa kutumia sauti yake kwenye sekunde 90 za wimbo huo. Sample ni kutoka kwenye wimbo ‘Gypsy Life on the Road’ uliachiwa Marekani mwaka 1997. Alikuwa akitaka alipwe fidia kutokana na kutumika bila ridhaa yake.

Mitsou alifungua kesi hiyo chini ya sheria za haki za kiraia (Civil Rights Law) sababu Drunk In Love ilitumika kwa madhumuni ya promotion na tangazo kwenye kipindi cha HBO kilichoonesha ziara yao ya On the Run Tour.

Kwenye maamuzi yake, jaji wa mahakama Manhattan, Cynthia Kern alisema kuwa haki za kiraia hazihusiani na kazi za maandishi na sanaa.

It is undisputed that the ‘Drunk in Love’ song and video are works of artistic expression and, pursuant to well established law, they are therefore exempted from the Civil Rights Law,” hukumu ya Kern ilisema.

Wimbo huo unapatikana kwenye album ya Beyonce yenye jina lake.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment