Kitendo cha kupupuruka mwili nikawa kama AT kwangu itakuwa ni fedheha kubwa sana– Asema Msechu


Peter Msechu hana mpango wa kupungua mwili ili awaridhishe mashabiki ambao wamekuwa wakimsema kutokana na kujiachia sana mwili.



Muimbaji huyo wa ‘Nyota’ anaamini kuwa mwonekano alionao sasa ni moja ya utambulisho wake, hivyo akipungua mwili inaweza kuharibu ‘image’ yake. Mfano wa anachokimaanisha hapo ni kama Baghdad wa zamani na alivyo sasa unaweza kumsahau baada ya kupungua sana.



Kushoto Baghdad wa sasa, kulia wa zamani
“Mi ninachokiogopa kwenye maisha yangu ni kuwa model, sababu nadhani ndio nitapoteza kabisa ile kitu ambayo watu wananijulia mimi.” Amesema Msechu kupitia 255 ya XXL.

Msechu amekiri kuwa ameshalalamikiwa na mashabiki wengi kuhusu alivyojiacha mwili, lakini msimamo wake ni kuendelea kubaki jinsi alivyo na kuwataka watu wapende muziki wake na sio mwili wake.

“Nishalalamikiwa sana sana sana na watu kuwa model lakini bado kuna image yangu ambayo mi naijua ipo ambayo nimekuwa nayo kwa muda mrefu sana, kwahiyo kitendo cha kupupuruka nikawa kama AT kwangu itakuwa ni fedheha kubwa sana, atabakia AT atabakia Msechu image lazima ibakie pale pale, nachoamini niko fiti nafanya kazi zangu, mi nishawaambaga watu wapende muziki wangu wasipende ninachokifanya mimi.”

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment