Joh Makini aeleza alichokuwa amepanga kufanya kama AKA asingetokea wakati wa kushoot video ya ‘Don’t Bother’



Tumekuwa tukishuhudia baadhi ya wasanii wakilazimika kushoot video bila wasanii waliowashirikisha kwenye nyimbo zao, kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo wasanii walioshirikishwa kukosa muda wa kushiriki kwenye video, au kushindwa kuelewana au tu kuamua kuzingua.



Ili kukabiliana na changamoto kama hizo, rapper wa Weusi Joh Makini alijipanga kikamilifu wakati anaenda Afrika Kusini kushoot video ya collabo yake na AKA ‘Don’t Bother’.

Joh amesema kuwa aliandaa version mbili ya wimbo huo ili ikitokea imeshindikana AKA kutokea kwenye video angeshoot version aliyoimba mwenyewe wimbo mzima.

“Mimi nilienda South Africa na ngoma version mbili ya ‘Don’t Bother’, ambayo niko mwenyewe na ambayo yeye (AKA) yuko, kwamba akizingua tunashoot hii. Lazima uwe tayari wakati mwingine huwezi kujua, lakini bahati nzuri jamaa alikuwa on time akaja tukashoot video.” Alisema Joh kupitia AYO TV.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment