Mwana FA: Msanii kutoa album ni kitu cha lazima



Mwana FA ni miongoni mwa wasanii wa kitambo ambao hadi sasa wanaendelea kufanya muziki, tena kwa upande wake ameanza kufanya kwa level za kuelekea kimataifa.


FA ambaye ameachia wimbo wake mpya ‘Asanteni Kwa Kuja’, wimbo ambao video yake imefanyika Afrika Kusini, ametoa msimamo wake kuhusu umuhimu wa album kwa msanii.

“Kufanyika albam ni lazima lakini tuje na idea ni jinsi gani tutauza, tunaweza kuifanya hii kazi ya distribution wenyewe, au tunaweza kuwafikia wale watu ambao wahindi hawawafikii, ninachofikiri si tumekwama, hatukuwa na invest ment kwenye muziki au hatujafungua vichwa vyetu” alisema FA kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio.

Pia Binamu ameigusia tofauti ya muziki wa sasa na ilivyokuwa enzi za ‘Ingekuwa Vipi’.

“Si tulianza muziki kipindi ambacho hatukuwa tunaamini kwamba muziki utatuingizia hata elfu kumi, sasa hivi hatuna wasanii wengi wa kutoa albam wanahesabika”, alisema Mwana FA.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment