Majibu ya bondia Manny Pacquiao kuhusu kustaafu ngumi



Mcheza ngumi raia wa Ufilipino ambaye amejizolea umaarufu duniani Manny Pacquiao amesema kwasasa anatarajia kustaafu mchezo huo April 2016 baada ya kumaliza pambano lake na bondia Timothy Bradley.



Bondia huyo tayari ameshinda mataji nane ya ubingwa wa dunia kwa sasa nia yake ni kuwania nafasi za juu za uongozi katika nchi yake ya Ufilipino anaamini ana nafasi kubwa ya kuiongoza nchi hiyo.

Pacquiao atapanda ulingoni kupambana na bondia huyo kutoka America kwa mara ya tatu April 9, 2016 hii ikiwa ni baada ya kushindwa kumpiga mpinzani wake mkubwa Floyd Mayweather katika pambano lililofanyika Las Vegas mwaka jana.

“Natarajia kustaafu ngumi na kujikita zaidi kwenye mambo ya siasa, pambano langu la mwisho litakuwa dhidi ya Timothy” alisema Pacquiao katika mahojiano.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment