Mpango wa Beyonce kufanya movie hii wakosolewa vikali Afrika




Kwa wengine Queen Bey hawezi kufanya kitu kibaya, lakini ukitoa mradi mpya wa filamu anaodaiwa kupewa.



Hivi karibuni kulikuwa na taarifa kuwa BeyoncĂ© anaweza kushiriki kwenye filamu ya historia ya Saartjie (“Sarah”) Baartman, mwanamke wa Afrika Kusini aliyenyonywa na Waingereza katika karne ya 18 na 19.




Baartman, aliyejulikana pia kama Hottentot Venus alikuwa akioneshwa hadharani akiwa mtupu kutokana na kuwa na makalio makubwa.

Chief Jean Burgess wa Afrika Kusini amedai kuwa Beyoncé hafai kuwakilisha mtu huyo muhimu kwenye historia ya nchi hiyo.

“She lacks the basic human dignity to be worthy of writing Sarah’s story, let alone playing the part,” Burgess, chifu wa Ghonaqua First Peoples, aliuambia mtandao wa News24.

“Ignoring the fact that the KhoiKhoi is alive and that Sarah’s story would have an impact on how we are portrayed, is a mistake of great magnitude.”

Burgess alisema kuwa ni vyema Beyonce akawekeza jitihada zake katika kuelezea historia ya mwanamke wa Kimarekani na sio Afrika.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment