Shilole: Nikiongea yaliyonitokea na Nuh mtaumia sana (Exclusive Video)





Shilole na Nuh Mziwanda wameuvunja rasmi uchumba wao uliodumu kwa takriban miaka mitatu.



“Mimi naye it’s over,” Shilole ameiambia Bongo5. “Basi tu kuna vitu vingi vimetokea, siwezi tu kuwa naye tena. Nitapenda tena lakini ntaangalia mtu ambaye tunaweza kuendana, uelewa wa akili, uelewa wa kila kitu,” ameongeza.

Shishi amesema alimvumilia sana Nuh lakini uvumilivu ulimshinda.
“Ni kuamua tu, vitu vinapozidi kuwa vingi halafu, unajua sisi wanawake Mungu ametupa kitu fulani kwamba tuwatunze nyinyi wanaume na sisi huwa tuna upendo sana, tuna uvumilivu wa vitu vingi sana lakini kuna wakati Mungu naye anakuja kukupa moyo kwamba nadhani tu hapa pumzika, acha, ndicho kilichonikuta mimi.”

“Sababu yaliyonitokea ni makubwa, siwezi kuongea kiukweli lakini nikiongea watu mtaumia sana. Siwezi kuongea ila mimi moyo wangu umeridhika.”

Shilole amesema kwa sasa yupo single and ready to mingle!


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment