Mido atimuliwa kazi ya ukocha Zamalek



Aliyekuwa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Misri na vilabu vya Tottenham pamoja na Middlesborough Mido amefutwa kazi kama mkufunzi wa Zamalek kwa mara ya pili baada ya siku 37 akiongoza mabingwa hao wa Misri.



Mido mwenye miaka 32 ambaye aliifundisha klabu hiyo kwa miezi 6 mwaka 2014 aliajiriwa tena tarehe 4 mwezi Januari.
Alishinda mechi zake nne za kwanza,lakini sare moja na kushindwa mara moja na baadaye kufuatiwa kushindwa 2-0 na wapinzani Al Ahly siku ya jumanne.

Hatua hiyo imeifanya Al Ahly ikiwa pointi saba juu ya Zamalek katika kilele cha jedwali la ligi ya taifa hilo.
Mohamed Salah sasa amechukua ukufunzi wa kilabu hiyo kama kaimu kocha huku kilabu hiyo ikitafuta kocha mpya ugenini.
Mkurungezi wa soka Hazem Emam,ambaye aliajiriwa wakati huohuo na Mido pia amepigwa kalamu.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment