Msanii wa muziki Linah Sanga amesema wasanii wengi wa kike wanashindwa kufanikiwa kutokana na kutokuwa serious na kile wanachokifanya.
Linah (kushoto) akiwa na rafiki yake Recho
Akizungumza katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM Jumatatu hii, Linah alisema hali hiyo inawafanya kutothamini kile wanachokifanya.
“Tumekuwa hatuko real,” alisema Linah.
“Unafiki wa maneno tu, huyu kampelekea huyu, huyu kampeleka huyu. Mara kutengenezeana stori. Halafu vitu vingine zinakuwa sio vya kweli, ukiwa karibu na mtu fulani mwingine anaona bora akakuharibie, yaani kuna vitu vinaendelea chini ya kapeti tunafanyiana sisi wasanii vinakuwa sio poa. Hiyo hali inapelekea tunakuwa hatusapotiani,ndio maana muziki wetu hauendelei,” aliongeza Linah.
Credit Bongo5
0 comments:
Post a Comment