Matokeo ya Klabu Bingwa Ulaya hatua ya 16 mechi zilizo chezwa February 16



Michuano ya Klabu Bingwa Ulaya hatua ya 16 bora ya imechezwa usiku wa February 16 kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja vya Parc des Princes na Estádio da Luz, michezo miwili iliyopigwa usiku huo ni mchezo, kati ya Benfica dhidi ya Zenit St. Petersburg na mchezo wa PSG dhidi ya Chelsea.



Klabu ya PSG kutoka Ufaransa imepata ushindi dhidi ya Chelsea mechi ya mkondo wa kwanza huku Benfica nao wakilaza Zenit St-Petersburg.



Chelsea wamefungwa 2-1 ugenini Paris.

Paris St-Germain walikuwa wakwanza kupata bao kupitia mshambuliaji matata wa Sweden Zlatan Ibrahimovic dakika ya 39.

Chelsea walisawazisha katika dakika ya 45 kupitia kwa Mikel Obi lakini Edison Cavan akaitumia dakika ya 78 kuwaumiza Chelsea.



John Obi Mikel hilo ndilo lilikuwa bao lake la sita kufungia Chelsea katika miaka 10 aliyokaa katika klabu hiyo ya Uingereza.


Kocha wa zamani wa PSG na Chelsea Carlo Ancelotti alikuwepo uwanjani kushuhudia timu zake za zamani


Nyota wa zamani wa Real Madrid na Brazil Ronaldo naye alikuwepo uwanjani

Benfica walipata bao pekee, wakiwa nyumbani, lilifungwa na Jonas katika muda wa ziada kutokana na mkwaju wa adhabu uliopigwa na Nicolas Gaitan.


Benfica forward Jonas Oliveira (right) celebrates after scoring a late winner against Zenit at home




Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment