Riyama ni wife material – Mysterio
Msanii wa muziki Leo Mysterio ambaye ni mchumba wa malkia wa filamu nchini Riyama Ally, amesema Riyama ni mwanamke mwenye sifa alizokuwa anazitafuta.
Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo Jumatano hii, Mysterio alisema muda wowote kuanzia sasa wanaweza kufunga ndoa kwani hatua za awali tayari wameanza kuzifanya.
“Unapopata mtu anayestahili kuwa mke usicheleweshe kufanya maamuzi ya kumuweka ndani.” alisema.
Aliongeza, “Unajua Riyana ni mtu ambaye ana huruma sana, ana akili pia ana mapenzi ya kweli kwangu na amekuwa akinisaidia katika kazi zangu hivyo nimefikia wakati nimeona ni bora nimuweke ndani kwani nimeridhika na yeye kwa kila kitu, ndiyo maana sijataka kuchelewesha kwa sababu yeye ndiye mwenye sifa kwangu,” alisiongeza.
Aidha, Mystereo amesema hajakurupuka katika maamuzi sababu yeye tayari alishafahamiana na Riyama Ally kwa zaidi ya miaka kumi uliyopita.
0 comments:
Post a Comment