Shirikisho la soka nchini Kenya (FKF) lapata Rais mpya
Shirikisho la soka nchini Kenya (FKF) limefanya uchaguzi wake mkuu na kupata Rais mpya ambaye alikuwa mwenyekiti wa klabu ya Kariobangi Sharks inayocheza ligi ya daraja ya chini nchini Kenya Nicholas Mwendwa.
Mwendwa amechaguliwa kwenye uchaguzi wa taifa wa shirikisho hilo ambao ulifanyika Kasarani, Nairobi. Aliungwa mkono na wajumbe 50 kati ya wajumbe wote 77 na kuwashinda Bw Ambrose Rachier na Ssemi Aina.
Aliyekuwa rais kwa miaka minne, Sam Nyamweya, alijiondoa kutoka kwenye uchaguzi muda mfupi kabla ya kura kupigwa.
0 comments:
Post a Comment