Yamoto Band kuachia albamu yao ya kwanza



Bendi ya muziki Yamoto Band, baada ya kufanya vizuri na kazi zao nyingi, inatarajia kuachia albamu yake ya kwanza hivi karibubuni.



Akizungumza na Bongo5 Jumatatu hii, Mkurugenzi wa Yamoto Band, Said Fella amesema mpango wa ujio wa albamu hiyo umekamilika.

“Kusema kweli albamu ipo tayari, sema tulikuwa kwenye mgongano kuhusu kulipa vati ya TRA ya asilimia 18, kwa sababu wasambazaji walikuwa wanataka tulipe sisi 18% yote, lakini tukawaambia tunatakiwa tugawane, kwa hiyo ndo tupo kwenye mazungumzo ya mwisho,” alisema Fella.

Aliongeza, “Nadhani mazungumzo yakikamilika tutawatangazia mashabiki rasmi, itapatikana wapi na bei zake, lakini wajue albamu ipo tayari,”

Credit bongo5

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment