Wanajeshi wa Uingereza watua Somalia


Wanajeshi hao wa Uingereza watasaidia wanajeshi wa AU

Wanajeshi wa Uingereza wamewasili nchini Somalia kusaidia katika juhudi za kukabiliana na wapiganaji wa Kiislamu wa al-Shabaab.

Wanajeshi hao ni sehemu ya kikosi cha Umoja wa Mataifa.

Wanajeshi waliowasili Somalia ni 10 na watasaidia kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika (Amisom) kukabiliana na al-Shabaab.

Idadi ya wanajeshi wa Uingereza nchini Somalia inatarajiwa kupanda hadi 70 sana wakihusika na shughuli za matibabu, mipango na uhandisi.

Wapiganaji wa al-Shabaab wamekuwa wakikabiliana na serikali ya Somalia kudhibiti maeneo ya nchi hiyo.

Wamekuwa wakitekeleza msururu wa mashambulio ndani ya nchi na pia nje ya nchi, hasa katika nchi jirani ya Kenya.

Kundi hilo linakadiriwa kuwa na wapiganaji kati ya 7,000 na 9,000.

Kikosi cha Amisom kilizinduliwa mwaka 2007 na kina wanajeshi kutoka Uganda, Burundi, Djibouti, Kenya na Ethiopia.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment