Rais Magufuli amwapisha Mkuu mpya wa mkoa wa Arusha.




Mkuu mpya wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amekula kiapo cha kuutumikia wadhifa huo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ,huku akielezea namna ya kudhibiti matukio ya shule kuungua moto yanayoutikisa mkoa huo.

Akizungumzia vipaumbele vyake mara baada ya kuapishwa Bwana Gambo amesema kwa sasa ataendelea kuunga mkono na kutekeleza maagizo ya Rais hususani katika usimamizi wa rasilimali fedha sambamba na kuleta unafuu wa maisha hususani kwa wananchi wa kipato cha chini.

katika hatua nyingine serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh Seleman Jaffo amewataka wakuu wote wa mikoa nchini kuanza zoezi la kuhakiki majina ya watumishi wote katika mikoa yao wanaodaiwa kuwepo masomoni ili kubaini majina hewa.

Hafla hiyo ya kuapishwa kwa mkuu huyo mpya wa mkoa wa Arusha umehudhuriwa na viongozi waandamizi wa serikali wakiongozwa na Makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassan na Waziri mkuu mh Majaliwa Kassimu Majaliwa.

katika tukio jingine Rais dkt John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt Donald Kaberuka Ikulu jijini Dar es Salaam ambaye hakusita kuizungumzia Tanzania ya kesho chini ya uongozi wa rais dkt john pombe magufuli na kusema kuwa anaiona Tanzania mpya yenye mafanikio makubwa.

Source ITV














Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment