G-Nako aeleza sababu za kusogeza kuachia video yake mpya ‘Original’ iliyokuwa itoke mwaka jana




Weusi walipanga kuumaliza mwaka 2015 kwa kuachia nyimbo tatu, ambapo walifanikiwa kuachia ‘Don’t Bother’ ya Joh Makini aliyomshirikisha AKA na nyingine ya Nikki Wa Pili ‘Baba Swalehe’.




Single ya G-Nako ‘Original’ ambayo ndio ingekamilisha ahadi yao ya nyimbo tatu haikufanikiwa kutoka mwaka uliopita kutokana na msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka kuvuruga mipango iliyokuwepo.

Video ya wimbo huo iliyofanyika Afrika Kusini chini ya muongozaji Justin Campos wa Gorilla Films imekamilika toka mwaka jana.

“Video tuliisogeza mbele kidogo kutokana kwamba ilikuwa kipindi cha sikukuu tukaona concentration itakuwa ndogo,” G-Nako ameieleza Bongo5.

Sababu nyingine ya kusogeza kuiachia amesema “lakini vile vile kuna baadhi ya channel za nje zilikuwa hazipokei kazi katika kipindi cha sikukuu.”

G-Wara wara amesema anatarajia kuanzia katikati ya mwezi huu video hiyo itakuwa imetoka na itaanzia channel ya nje ambayo hakusema ni ipi.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment